Biden alaani shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine
Biden alaani shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden amelaani shambulizi la Urusi dhidi ya Ukraine, akisema Moscow "haitafanikiwa" katika vita vyake vinavyoendelea.
Alisema Washington itaendelea kuunga mkono gridi ya nishati ya Ukraine.
"Ninalaani, kwa nguvu zote, kuendelea kwa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na juhudi zake za kuwatumbukiza gizani watu wa Ukraine,"Biden alisema katika chapisho kwenye X.
"Urusi haitafanikiwa kamwe nchini Ukraine, na roho ya watu wa Ukraine haitavunjika kamwe."
Wakati huo huo Rais wa Ukraine anaomba Uingereza, Marekani na washirika wengine kutoa idhini kwa Ukraine kutumia silaha zilizotengenezwa na nchi za magharibi, za masafa marefu kushambulia maghala ya risasi, ndege na viwanja vya ndege ndani kabisa ya Urusi.
Comments
Post a Comment