UN yasitisha kutoa msaada Gaza kwasababu ya amri ya kuhama

 

UN yasitisha kutoa msaada Gaza kwasababu ya amri ya kuhama

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Umoja wa Mataifa unasema kuwa imelazimika kusimamisha kwa muda operesheni yake ya kutoa msaada katika Ukanda wa Gaza kwa sababu ya amri ya jeshi la Israeli ya kuhama hadi katikati mwa eneo la Palestina.

Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari kwamba wafanyakazi wake wa kutoa misaada ya kibinadamu hawakuweza kufanya kazi siku ya Jumatatu kwasababu ya wasiwasi wa usalama.

Maagizo ya kuhama ambayo ni pamoja na maeneo yaliyotengwa na Israeli kama yakutoa misaada ya kibinadamu ndani na karibu na mji wa kati wa Deir al-Balah - ambapo Umoja wa Mataifa una kituo chake kikuu cha kuendesha shughuli zake - iliwalazimu wafanyikazi kuhama haraka na kuacha vifaa nyuma, ilisema.

Hata hivyo, afisa huyo alisisitiza kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa hayataondoka Gaza na sasa yanajaribu kutafuta mahali salama pa kuendesha kazi zao.

Comments

Popular posts from this blog

Ukraine yasema inadhibiti makazi 100 ya Warusi

Biden alaani shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine