Posts

Showing posts from August, 2024

Wanajeshi wa Kiukreni wajisalimisha: hali katika Mkoa wa Kursk

Image
 Wanajeshi wa Kiukreni wajisalimisha: hali katika Mkoa wa Kursk Kwa jumla, Kiev imepoteza hadi wafanyakazi 7,000 tangu mapigano yaanze katika eneo hilo MOSCOW, Agosti 28. . Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimepoteza hadi wanajeshi 380 na magari 30 ya kivita katika mwelekeo wa Kursk katika siku iliyopita, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema. Kulingana na shirika hilo, wanajeshi watano wa Kiukreni wamejisalimisha. Kwa jumla, Kiev imepoteza hadi wafanyakazi 7,000 tangu mapigano yaanze katika eneo hilo. TASS imekusanya habari muhimu kuhusu hali inayojitokeza. Operesheni ya kupunguza vikosi vya Kiukreni - Kikosi cha vita cha Kaskazini, kikisaidiwa na jeshi la anga na ufyatuaji wa risasi, kilirudisha nyuma mashambulio manane ya vikundi vya shambulio la adui kuelekea Borki, Korenevo, Kremyanoye na Malaya Loknya. - Jeshi la Urusi pia lilizuia majaribio ya mashambulizi ya Spalnoye, Olgovka na Russkaya Konopelka. - Viwango vya Kiukreni vya wafanyikazi na vifaa katika maeneo ya Apanasovka, Borki...

Zelensky asema atawasilisha mpango kwa Marekani kuhusu namna ya kumaliza vita

Image
  Zelensky asema atawasilisha mpango kwa Marekani kuhusu namna ya kumaliza vita CHANZO CHA PICHA, REUTERS Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema atawasilisha mpango kwa Marekani kuhusu jinsi anavyodhamiria kumaliza vita na Urusi. Zelensky, ambaye amezungumza na waandishi wa habari kuadhimisha siku ya uhuru wa Ukraine ambayo ilikuwa Jumamosi, anasema atawasilisha mpango huo kwa wagombea urais Kamala Harris na Donald Trump, pamoja na Rais wa sasa Joe Biden. Mpango huo utajumuisha hatua katika nyanja za kidiplomasia na kiuchumi, anasema, tofauti na uvamizi wa Ukraine huko Kursk, ambao pia umekuwa sehemu ya mkakati wa kuifanya Moscow kuanza mazungumzo ya amani. Zelensky pia anauambia mkutano wa wanahabari mjini Kyiv kwamba Ukraine ilifanya jaribio la kwanza la kombora la balestiki lililotengenezwa nchini humo. Ukraine tayari imetumia baadhi ya makombora ya balistiki dhidi ya Urusi ambayo yalitolewa na Marekani.

Ukraine yasema inadhibiti makazi 100 ya Warusi

Image
  Ukraine yasema inadhibiti makazi 100 ya Warusi Ukraine inaendelea na mashambulizi yake katika eneo la Kursk la Urusi, kamanda mkuu wa kijeshi wa Kyiv anasema. Jenerali Oleksandr Syrskyi anasema wanajeshi wa Ukraine wanadhibiti kilomita za mraba 1,294 (maili za mraba 500) za eneo la Urusi na makazi 100. Takribani wanajeshi 594 wa Urusi walichukuliwa mateka, anaongeza. Wiki iliyopita, Rais Zelensky alisema Ukraine inadhibiti zaidi ya kilomita za mraba 1,250 za eneo la Urusi. Akiongea kupitia Televisheni ya Ukraine, Syrskyi anasema moja ya malengo ya uvamizi wa Ukraine huko Kursk ilikuwa "kuvuruga idadi kubwa ya wanajeshi wa adui kutoka maeneo mengine", kama vile Pokrovsk na Kurakhove huko Donbas, na ilifikiwa kwa mafanikio. Anaongeza kuwa Urusi ilifahamu lengo hili na "inazingatia vitengo vyake vilivyo tayari kupambana katika eneo la Pokrovsk".

Uhalifu wa mtandaoni Nigeria: Kundi la walaghai wa Black Axe lapata pigo

Image
  Uhalifu wa mtandaoni Nigeria: Kundi la walaghai wa Black Axe lapata pigo CHANZO CHA PICHA, INTERPOL Maelezo ya picha, Operesheni za kukabiliana na genge la Black Axe zilielekezwa Uswizi ambapo watu walikamatwa nchini Uswizi Maelezo kuhusu taarifa Author, Charlie Northcott Nafasi, BBC Africa Eye Saa 1 iliyopita Vitengo vya polisi kote duniani vimeungana katika msururu wa operesheni za siri zinazolenga mojawapo ya mtandao unaoogopwa zaidi wa uhalifu Afrika Magharibi - Black Axe. Operesheni kwa jina Jackal III ilishuhudia maafisa waliovaa nguo maalum zinazovaliwa na polisi au wanajeshi kwa ajili ya ulinzi katika nchi 21 kati ya Aprili na Julai 2024. Operesheni hiyo iliyoratibiwa na shirika la polisi wa kimataifa Interpol, ilisababisha kukamatwa kwa watu 300 wenye uhusiano na mtandao wa Black Axe na makundi mengine tanzu. Interpol iliita operesheni hiyo "pigo kubwa" kwa mtandao wa uhalifu wa Nigeria, lakini ilionya kwamba kufikia kwake kimataifa na ustadi wa teknolojia unamaani...

Biden alaani shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine

Image
  Biden alaani shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine CHANZO CHA PICHA, EPA Rais wa Marekani Joe Biden amelaani shambulizi la Urusi dhidi ya Ukraine, akisema Moscow "haitafanikiwa" katika vita vyake vinavyoendelea. Alisema Washington itaendelea kuunga mkono gridi ya nishati ya Ukraine. "Ninalaani, kwa nguvu zote, kuendelea kwa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na juhudi zake za kuwatumbukiza gizani watu wa Ukraine,"Biden alisema katika chapisho kwenye X. "Urusi haitafanikiwa kamwe nchini Ukraine, na roho ya watu wa Ukraine haitavunjika kamwe." Wakati huo huo Rais wa Ukraine anaomba Uingereza, Marekani na washirika wengine kutoa idhini kwa Ukraine kutumia silaha zilizotengenezwa na nchi za magharibi, za masafa marefu kushambulia maghala ya risasi, ndege na viwanja vya ndege ndani kabisa ya Urusi.

UN yasitisha kutoa msaada Gaza kwasababu ya amri ya kuhama

Image
  UN yasitisha kutoa msaada Gaza kwasababu ya amri ya kuhama CHANZO CHA PICHA, REUTERS Umoja wa Mataifa unasema kuwa imelazimika kusimamisha kwa muda operesheni yake ya kutoa msaada katika Ukanda wa Gaza kwa sababu ya amri ya jeshi la Israeli ya kuhama hadi katikati mwa eneo la Palestina. Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari kwamba wafanyakazi wake wa kutoa misaada ya kibinadamu hawakuweza kufanya kazi siku ya Jumatatu kwasababu ya wasiwasi wa usalama. Maagizo ya kuhama ambayo ni pamoja na maeneo yaliyotengwa na Israeli kama yakutoa misaada ya kibinadamu ndani na karibu na mji wa kati wa Deir al-Balah - ambapo Umoja wa Mataifa una kituo chake kikuu cha kuendesha shughuli zake - iliwalazimu wafanyikazi kuhama haraka na kuacha vifaa nyuma, ilisema. Hata hivyo, afisa huyo alisisitiza kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa hayataondoka Gaza na sasa yanajaribu kutafuta mahali salama pa kuendesha kazi zao.

"Tutajibu shambulio la Urusi," Zelensky asema

Image
  "Tutajibu shambulio la Urusi," Zelensky asema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kuwa Kyiv italipiza kisasi baada ya nchi hiyo kukumbwa na duru nyingine ya mashambulizi ya Urusi usiku kucha. Anasema shughuli za uokoaji zinaendelea, lakini watu wanne wameuawa na wengine 16 kujeruhiwa katika mashambulizi hayo. Urusi ilishambulia "zaidi ya shabaha 90 za angani dhidi ya raia na miundombinu", anasema, zikiwemo ndege zisizo na rubani 81, na makombora ya masafa marefu, ya balestiki na ya kurushwa angani. "Bila shaka tutaijibu Urusi kwa mashambulizi haya na mengine yote. Uhalifu dhidi ya binadamu hauwezi kwenda bila kuadhibiwa," Zelensky aliongeza katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii.

Dakika 18 zilizopitaMashambulizi ya Urusi nchini Ukraine: Tunachojua kufikia sasa

Image
  Mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine: Tunachojua kufikia sasa CHANZO CHA PICHA, REUTERS Urusi iliilenga Ukraine kwa wimbi jingine la mashambulizi usiku kucha, huku maafisa wa Ukraine wakiripoti kuwa takribani watu wanne waliuawa. Tahadhari za uvamizi wa anga zilitolewa mapema asubuhi, wakati wachunguzi wa Ukraine wapoligundua ndege ya Kirusi ikirusha kombora la hypersonic. Miundombinu ya kiraia ilipigwa katika mji wa mashariki wa Kryvyi Rih siku ya Jumatatu, na kuua watu wawili. Watu kadhaa hawajulikani walipo Mkuu wa mkoa wa Zaporizhzhia Ivan Fedorov alisema mtu mmoja ameuawa na mwanaume na mwanamke kujeruhiwa katika mji wa Zaporizhzhia. Milipuko pia imeripotiwa katika mikoa ya Kyiv, Sumy, Khmelnytsky na Mykolayiv. Mashambulizi hayo yanajiri siku moja baada ya Urusi kuishambulia Ukraine kuwa mojawapo ya mashambulizi makubwa zaidi ya anga katika vita hivyo, na kuua takribani watu saba na kujeruhi makumi ya wengine, huku umeme ukikatika katika miji mingi.

Mfungwa kijana wa Ujerumani aliyebadilishwa na muuaji wa Urusi

Image
  Mfungwa kijana wa Ujerumani aliyebadilishwa na muuaji wa Urusi CHANZO CHA PICHA, LIK FAMILY Maelezo ya picha, Kevin Lik alipelekwa katika hospitali ya Ujerumani kwa uchunguzi baada ya kuachiliwa Maelezo kuhusu taarifa Author, Sergei Goryashko Nafasi, BBC Saa 3 zilizopita Kevin Lik (19) pamoja na mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, ni miongoni mwa watu 16 walioachiliwa na Urusi tarehe 1 Agosti, katika mpango wa kubadilishana wafungwa kati ya Marekani na nchi nyingine za Magharibi. Kijana huyo - mwenye uraia wa Urusi na Ujerumani - alikamatwa mwaka jana akiwa bado shuleni na akawa mtu mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Urusi ya sasa kuhukumiwa kwa uhaini. Kevin alizaliwa mwaka 2005 huko Montabaur, mji mdogo magharibi mwa Ujerumani. Mama yake Mrusi, Victoria, aliolewa na raia wa Ujerumani, ingawa ndoa haikudumu, yeye na mwanawe walibaki Ujerumani. Walitembelea Urusi kila baada ya miaka kadhaa hadi Victoria alipoamua kurudi moja kwa moja. Kevin alikuwa na umri w...